@Tuko

Michelle asimulia alivyokasirishwa na Obama wakati wa deti yao ya kwanza

1 months ago, 15 Nov 12:56

By: Mwangi Muraguri

-Kulingana na Michelle, haikumpiga mshipa kuwa ataishia kuwa mume wa Barack Obama

-Hata hivyo, Michelle anakiri kuvutiwa zaidi na sauti ya Obama, upole na maono yake

-Alisema Obama alivuta sigara baada ya miadi yao ya kwanza, jambo lililomghasi sana

Michelle na Barack Obama walikutana mara ya kwanza wakati Michelle alipopewa jukumu la kumpa mwongozo Obama katika kampuni moja ya Uanasheria iliyokuwa Chicago.

Licha ya sifa za Obama kuzagaa kote kama mwanafunzi na kiongozi chipukizi, Michelle anasema hakuvutiwa naye alipomuona kwenye picha kwa mara ya kwanza.

Michelle anakiri kuwa kando na sauti "nzuri na ya kuvutia" walipozungumza kwa simu na Obama kwa mara ya kwanza kabla ya kuonana ana kwa ana, hakuhisi jambo jingine lililompendeza .

Habari Nyingine:

Aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama. Picha: UGC

Hatimaye, Michelle anaeleza kuwa alianza kutamani kumjua Obama zaidi na hatimaye wakaishia kuwa wapenzi.

" Ukweli ni kwamba, uhusiano kati yetu ulikuwa umeanza kushamiri," alisema Michelle akiongeza alivyofurahia kila walipokutana ndani ya nje ya afisi.

Habari Nyingine:

Barack Obama na mkewe Michelle wakiwa na mabinti zao wawili Malia na Sasha. Picha: Barack Obama/Facebook

Aidha, katika kitabu cha Becoming kinachosimulia matukio muhimu katika maisha yake, Michelle anasema haikumpiga mshipa kuwa Obama angeishia kuwa mumewe.

" Sikuwahi kufikiria hata mara moja kuwa angeishia kuwa mpenzi wangu. Kwanza miye ndiye niliyejukumika kumpa mwongozo. Aidha, karibuni nilikuwa nimeapa kuwa sitojihusisha na mapenzi, maana nilikuwa nimeshikika sana kikazi," alisema Michelle.

Hata hivyo, Michelle anaeleza kuwa azma yake ya kumuepuka Obama iligonga mwamba kwa kuwa Obama alikuwa na tamanio kuu la wao kuwa wapenzi.

Habari Nyingine:

Michelle Obama na mabinti zake wawili Sasha Obama na Malia Obama. Picha: Michelle Obama/Facebook

Michelle anayemtaja Obama kama mwanaume anayevutia, mpole na mwenye maono anasema kuwa baada ya "busu la kwanza", uhusiano kati yake na Obama ulishamiri huku " akikabwa na kiu kuu ya kumjua zaidi haraka iwezekanavyo"

Wawili hao walioana mwaka 1991 na wamejaliwa watoto wawili wa kike Sasha na Malia.

Kwenye kitabu hicho, Michelle anaelezea huzuni iliyomkabili baada ya mimba yake kuchoropoka na hivyo kuwalazimu ili kutunga mimba ya mabinti zake wawili Sasha na Malia.

Habari Nyingine:

Pia kitabu hicho kinaelezea jinsi alivyokumbana na ubaguzi wa rangi katika jumba la White House na hatamu yake kama Mama wa taifa wa kwanza mweusi.

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Read More

Category: topnews news

Suggested

3 hours ago, 12:43
@Tuko - By: Christopher Oyier
Afisa wa polisi apatikana na hatia ya kumuua mshukiwa aliyekuwa kizuizini

Afisa mkuu wa polisi wa kituo cha polisi cha Ruaraka Nahashon Mutua amepatikana na hatia ya kumdhulumu mshukiwa na kusababisha kifo chake. Mutua alikamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa mauaji ya Marti ...

Category: topnews news
3 hours ago, 12:22
@Tuko - By: Adia Mwikali
Lesbian signs: How to tell if a girl likes girls?

Just as there are signs for everything else, these★LESBIAN SIGNS★will help you figure out if your girlfriend is actually a lesbian and not just being nice. It will go a long way in ensuring that your ...

Category: topnews news
3 hours ago, 12:12
@Tuko - By: Lauryn Kusimba
Uhuru akanusha madai vita dhidi ya ufisadi vinawalenga viongozi Wakalenjin

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kwamba serikali yake haimlengi mtu yeyote wala kabila lolote inapopigana vita dhidi ya ufisadi.Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka. ...

Category: topnews news
4 hours ago, 11:51
@Tuko - By: Christopher Oyier
DCI yaombwa kuchunguza mauaji ya padre wa Kiambu na kuwakamata wahusika

Habari zimechipuka kuwa padre wa kanisa katoliki wa parokia ya Kinoo, kaunti ya Kiambu aliyeuawa, John Njoroge, hakuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya waumini wa kanisa hilo. Hayo yalifichuliwa kwenye ...

Category: topnews news
4 hours ago, 11:06
@Tuko - By: Ryan Mutuku
10 best goals that you actually want in your relationship

These ten most important ⭐RELATIONSHIP GOALS⭐ for couples will help you achieve your ambitions without interfering with each other. Make your relationship happy and healthy by adopting comfortable and ...

Category: topnews news
4 hours ago, 11:06
@Tuko - By: Christopher Oyier
Wetang'ula amchochea Uhuru kuunga mkono kura ya maoni na mabadiliko ya utawala

Seneta wa Bungoma Moses Wetang’ula amemshawishi Rais Uhuru Kenyatta kuunga mkono kura ya maoni na mabadiliko ya mfumo wa uongozi na utawala ili kudumisha amani na umoja yaliyopatikana nchini baada ya ...

Our App